Posts

Showing posts from April, 2024

HOSPITALI YA AGHAKHAN YAKAMILISHA MRADI WAKE

Image
Hospital ya Agha khan kwa ushirikiano na ubalozi wa  wa ufaransa nchini Kenya pamoja na serikali ya county ya Mombasa leo hii wameendeleza ufunguzi wa ultra model building ambayo imeendelezwa kutoka kuwa vitanda 86-115  na shirika la Agha khan network ambayo  inachukuwa hatua hizi ili kuhakikisha maisha yameboreshwa kutokana na kuboresha sekta ya afya Agha Khan Health Service Kenya imefanya sherehe ya kukamilisha mradi wa ukarabati wa Hospitali ya Aghakhan Mombasa, hatua muhimu katika ahadi yake ya kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa idadi ya watu 1.4 milioni katika kaunti ya mombasa na maeneo zaidi kupitia mfano wake wa kituo cha msingi na matawi ya vituo vya kutolea huduma. Hospitali iliyokarabatiwa hivi sasa imebadilishwa kutoka kituo cha vitanda 86 hadi kuwa taasisi ya afya ya sekondari yenye vitanda 115 vyenye huduma za kiafya zilizounganishwa kikamilifu kwa jamii inayohudumiwa. "Ningependa kupongeza kazi ambayo imefanywa na Aghakhan  na kaunti ya Mombasa kw...

ASKOFU WA KANISA LA KIANGLIKANA HAPA MOMBASA AWASIHI MADAKTARI KUSIMAMISHA MGOMO.

Image
Askofu wa kanisa la kianglikana hapa Mombasa Alphonce Baya amewasihi madaktari kueka maslahi yao chini na  kusimamisaha mgomo ambao umeingia siku ya 41 leo. Akihutubia wanahabari hapa Mombasa aakofu Baya amesema maisha ya wakennya ni muhimu zaidi ikilinganishwa na mahitaji yao madaktari mbayo yanaweza kuangaziwa pole pole. Kiongozi huyo wa dini aidha amewaomba madaktari warejee kazi huku wakitafuta suluhu ili  kuokoa maisha ya wagonjwa. 

WANAHARAKATI WA ANTI LGBTQ WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA MVITA CLINIQ

Image
Wanaharakati wa Anti LGBTQ wameweza kuendeleza maandamano yao katika hospitali ndogo ya mvita clinic hapo jana kupinga kutolewa kwa huduma za kina mama wajawazito na kuendeleza huduma za kuwatibu watu wenye jinsia moja katika hospitali hiyo. Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa vuguvugu hilo Salim Karama amesema kuwa Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswammad shariff Nasir   aliwaahidi kurudisha shughuli za kliniki hiyo alipowaita  kwenye  kikao ofisini kwake. Aidha Ameongezea kwa kusema kuwa wataendeleza maandamano yao  hadi pale agizo la gavana   la kurudisha maternity ya kina mama litatekelezwa.