MAFURIKO YAENDELEA KUSABABISHA MASAIBU
Idadi ya vifo kutokana na matukio yanayohusiana na mafuriko imeongezeka hadi 257, na kuashiria hasara ya watu 19 zaidi katika saa 24 zilizopita. Msemaji wa serikali Isaac Mwaura alisema watu wazima 14 na watoto watano waliripotiwa kufariki katika muda wa saa 24 zilizopita. Alisema idadi ya watu walioathirika na mvua kwa sasa ni 293,661 huku kaya 54,837 zikiwa zimekosa makazi. Mwaura alisema watu wengine 188 wamejeruhiwa. "Sisi vile vile tunahuzunishwa na kuongezeka kwa idadi ya vifo na tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia zilizoathiriwa," Mwaura alisema. Alisema miundombinu imeathiriwa sana na uharibifu mkubwa wa njia za reli na barabara nyingi hazipitiki. Mwaura alifichua kuwa wakati huo huo serikali inakusanya karibu Sh4 bilioni kusaidia juhudi za uokoaji na usaidizi na kusisitiza kujitolea kwa serikali kulinda maisha na mali ya Wakenya wote walioathiriwa. Mwaura alisema huduma za afya pia zimeathiriwa pakubwa,...