MAFURIKO YAENDELEA KUSABABISHA MASAIBU




Idadi ya vifo kutokana na matukio yanayohusiana na mafuriko imeongezeka hadi 257, na kuashiria hasara ya watu 19 zaidi katika saa 24 zilizopita.

 Msemaji wa serikali Isaac Mwaura alisema watu wazima 14 na watoto watano waliripotiwa kufariki katika muda wa saa 24 zilizopita.

 Alisema idadi ya watu walioathirika na mvua kwa sasa ni 293,661 huku kaya 54,837 zikiwa zimekosa makazi.


 Mwaura alisema watu wengine 188 wamejeruhiwa.

 "Sisi vile vile tunahuzunishwa na kuongezeka kwa idadi ya vifo na tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia zilizoathiriwa," Mwaura alisema.

 Alisema miundombinu imeathiriwa sana na uharibifu mkubwa wa njia za reli na barabara nyingi hazipitiki.

 Mwaura alifichua kuwa wakati huo huo serikali inakusanya karibu Sh4 bilioni kusaidia juhudi za uokoaji na usaidizi na kusisitiza kujitolea kwa serikali kulinda maisha na mali ya Wakenya wote walioathiriwa.

 Mwaura alisema huduma za afya pia zimeathiriwa pakubwa, huku vituo 61 vya afya vikiwa na matatizo katika kaunti 11.

 Kutokana na hali hiyo, alisema visa 44 vya kipindupindu vimeripotiwa kufikia sasa katika kaunti za Tana River na Marsabit ambapo maafisa wa Wizara ya Afya na Shirika la Msalaba Mwekundu wanaendesha mipango ya kuwafikia watu ili kukomesha kuenea kwa mkurupuko huo.

 "Katika kukabiliana na mgogoro huo, serikali inatekeleza kikamilifu mipango ya kudhibiti magonjwa yatokanayo na maji, ikiwa ni pamoja na juhudi za kudhibiti milipuko ya kipindupindu," Mwaura alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Nyayo House.

 Msemaji huyo alisema ukarabati unaoendelea wa miundombinu iliyoharibiwa unatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa Mei.

 Alisema serikali inafanyia kazi sehemu ya barabara muhimu ili kurejesha usafiri salama ambapo barabara zimeharibiwa na maji kujaa na kukatika.

 Alisema uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara ulitokea katika mikoa ya Nyanza, Magharibi, Pwani, Bonde la Ufa na Mashariki.

 Msemaji huyo wa serikali pia alifichua kuwa mabwawa 198 yametambuliwa kuwa hatari zaidi baada ya tathmini ya kitaifa.

 Alisema uhamishaji wa aina mbalimbali unaendelea katika mikoa iliyoathirika kufuatia agizo la rais lililotolewa Mei 2, 2024.

 "Hata hivyo, tunawashauri Wakenya wote kusalia salama na kuzingatia utabiri wa hali ya hewa na notisi za kuhama ambazo zinatolewa na serikali na mashirika mengine," Mwaura alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Premier Hospital’s Lenah Wangari Karuga Crowned Kenya’s Best Nurse Midwife at NMOYA Awards

SIMBA APPAREL EPZ UNVEILS NEW PRODUCTION FACILITY IN MOMBASA

ABE International Hosts Inaugural Student Entrepreneurship Summit in Mombasa"