WANAUCHUMI WAKONGAMANA MOMBASA KWA WARSHA YA SIKU TANO
Jumuiya ya kiuchumi ya kenya( ESK) leo hii wamefungua rasmi warsha itakayochukua siku tano jijini Mombasa huku dhima ya mwaka huu ikiwa ni kutoa uongozi kuelekea katika ukuaji wa uchumi nchini kenya.
Jumuiya hii inayoshirikisha wadau na wataalamu mbalimbali kutoka sekta muhimu za kiuchumi wamekongamana ili kutoa fursa na jukwaa kwa wanauchumi kutoka sekta mbalimbali katika kuyajadili maswala muhimu ya kiuchumi yanayokabili nchi.
Warsha hii imeongozwa na mkurugenzi
mkuu wa jumuiya hiyo Dunstone Ulwodi ambaye amesema. kwamba ipo haja kama wanauchumi kuunga mikono sera za kiuchumi zinazoweza kubadilisha nchi huku akisisitiza kwamba sharti sera za kiuchumi ziwe sera za kuleta mabadiliko katika uchumi.
"Tunasema kwamba sera lazima ziwe zinabadilisha nchi kwa uzuri,lazima ziwe sera za kuleta mabadilko katika uchumi wa nchi"
Aidha Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki Suleiman Shabhal alihudhiria Kongamano hilo na kusisitiza kwamba bara la afrika liko na mawazo tele katika uwekezaji lakini fursa za kuwekeza katika mawazo hayo ndio huwa ngumu sababu ya ukosefu wa kifedha ,Shabhal amesema kwamba ataidhinisha muswada katika bunge la afrika mashariki la (EALA) la kuweka benki ya uwekezaji itakayosaidia miradi inayokua ili kuifanya itekelezwe
Aidha amewashauri wanauchumi kuhimiza Sera za Ushirikiano wa Umma na Sekta za Binafsi (PPP) ili kuwezesha ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuvuta wawekezaji wengi akisema hatua hii ya pande zote mbili zinaweza kuleta ufanisi zaidi katika kutoa huduma kwa umma akisema kwamba hili halitawezekana kama wataiachia serikali peke yake bila kuhuzisha sekta za kibinafsi.
Comments
Post a Comment